Takriban watu wanne wameuawa katika tukio la kufyatua risasi kiholela katika sherehe ya kuzaliwa kwa mtoto huko California.
Wengine kumi walijeruhiwa kwa risasi kwenye mgahawa Jumamosi jioni, katika mji wa kaskazini mwa jimbo hilo wa Stockton.
Polisi wa eneo hilo wanasema waathiriwa ni pamoja na watu wazima na watoto. Hali za waliojeruhiwa hazijathibitishwa.
Mshukiwa bado hajakamatwa na polisi wanaamini kuwa shambulizi hilo la risasi "lilikusudiwa".
Chanzo; Bbc