Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Trump Kuwakataa Wahamiaji Kutoka Nchi Masikini

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema atasitisha kwa muda uhamiaji kutoka nchi alizozitaja kama “masikini,” ikiwa ni siku moja baada ya raia wa Afghanistan kudaiwa kuwapiga risasi na kuwaua wanajeshi wawili wa ulinzi wa taifa hilo.

Kupitia mtandao wake wa kijamii, Trump amesema atabatilisha maombi ya mamilioni ya wahamiaji yaliyoidhinishwa na utawala wa rais wa zamani, Joe Biden, hatua inayoongeza kasi ya msimamo wake mkali dhidi ya wahamiaji.

"Nitasitisha kabisa hatua ya wahamiaji kutoka nchi masikini kuingia Marekani ili mfumo uliopo upate nafuu dhidi ya mzigo mkubwa uliopo sasa," aliandika Trump kwenye mtandao wake wa X.

Trump alisema hatua hii imechukuliwa baada ya raia wa Afghanistan kudaiwa kuwapiga risasi walinzi wake wawili. Sarah Beckstrom, mwenye umri wa miaka 20 na mwanachama wa Jeshi la Taifa, alifariki dunia kutokana na majeraha aliyopata baada ya kushambuliwa mjini Washington. Askari mwingine, Andrew Wolfe (24), amejeruhiwa vibaya na bado amelazwa hospitalini.

Uchunguzi wa tukio la shambulio

Maafisa wa ujasusi wameanzisha uchunguzi wa tukio hilo na wamemtambua mshukiwa kuwa ni Rahmanullah Lakanwal, kijana wa miaka 29 aliyewahi kufanya kazi na kikosi cha Marekani cha Zero Units nchini Afghanistan kikosi kinachoshirikiana na shirika la ujasusi la Marekani (CIA) katika operesheni za kupambana na ugaidi. Hadi sasa, haijafahamika sababu ya mshukiwa kutekeleza shambulio hilo.

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: