Watoto 200 waliozaliwa kutokana na mfadhili wa mbegu za kiume wapo hatari kupata saratani.
Barani Ulaya na sehemu nyingine duniani, wasiwasi mkubwa umeibuka baada ya kubainika kuwa mfadhili mmoja wa mbegu za kiume kutoka Benki ya Manii ya Ulaya, ESB, nchini Denmark, aligunduliwa mwaka 2023 kuwa na mabadiliko adimu ya kijenetiki yanayoweza kuongeza hatari ya saratani ya utotoni.
Uchunguzi wa DW na washirika wa vyombo vya habari barani Ulaya unaonesha kuwa mamia ya watoto wanaweza kuwa wameathiriwa, huku baadhi ya wazazi wakisema hawakuwahi kufahamishwa kwa wakati kuhusu hatari hiyo.
Chanzo; Dw