Matangazo ya Jioni: Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekosolewa kuhusu matayarisho ya kuwapa askari polisi na wanajeshi risasi 120 kwa ajili ya kukabiliana na vurugu za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Januari mwakani.
Kauli ya Museveni imekosolewa na mpinzani wake mkuu Robert Kyagulanyi ambaye amewatahadharisha polisi na wanajeshi kwamba wasikubali kuwaua wananchi wenzao wakilinda maslahi ya kiongozi asiyeheshimu maisha ya binadamu.
Chanzo; Dw