Mwanaume wa umri wa makamo ameuawa na kundi la watu katika Kituo cha Ununuzi cha Mururi eneo Bunge la Gichugu, Kaunti ya Kirinyaga, baada ya kukamatwa akiiba kuku walioandaliwa kwa ajili ya kusherehekea Krismasi.
Kwa mujibu wa wakazi wakiongozwa na Francis Mutegi, kisa hicho kilitokea majira ya saa mbili asubuhi wakati mtuhumiwa alipoonekana ndani ya boma la msimamizi wa kijiji.
"Msimamizi wa kijiji alitoa tahadhari baada ya mwanae kumuona mwanaume akiweka kuku kwenye gunia kwenye banda la kuku. Alimwamsha, na kengele ikapigwa na kuwavutia wenyeji," Mutegi alisema.
Wakazi wanadai mshukiwa alikuwa tayari ameiba kutoka kwenye kaya zingine mbili, mapema usiku huo kabla ya kukamatwa.
Baada ya mwanaume huyo kukamatwa wananchi wenye hasira waliripotiwa kununua mafuta kwenye kituo cha mafuta kilichopo karibu na saa 24 na kumchoma moto mtuhumIwa huyo, kabla ya polisi kufika eneo la tukio.
Chanzo; Itv