Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Meta Yaanza Kuondoa Watoto Mtandaoni

Kampuni ya Meta imesema imeanza kuondoa akaunti za vijana walio chini ya umri wa miaka 16 kutoka kwa mitandao yao ya kijamii nchini Australia kuelekea marufuku iliyotangazwa na Serikali ya nchi hiyo kuwa watoto walio chini ya umri wa miaka 16 hawataruhusiwa kuwa na akaunti katika mitandao ya kijamii kama Tiktok, Facebook, Youtube na Instagram.

Sheria hiyo inaanza kutekelezwa rasmi Jumatano ijayo.

Kampuni hiyo kubwa ya teknolojia ilitangaza mwezi uliopita kuwa imeanza kuwafahamisha watumiaji wenye umri wa kati ya miaka 13 hadi 15 kwamba akaunti zao zitaanza kufungwa kuanzia Desemba 4, 2025.

Takriban watumiaji 150,000 wa Facebook na akaunti 350,000 za Instagram wanatarajiwa kuathirika.

Mitandao ya Threads, sawa na X, zinaweza kupatikana tu kupitia akaunti ya Instagram.

Marufuku ya kwanza duniani ya mitandao ya kijamii nchini Australia itaanza Disemba 10, huku kampuni zikikabiliwa na faini ya hadi A$49.5m (US$33m, £25m) iwapo zitashindwa kuchukua "hatua zinazofaa" kuwazuia watoto chini ya miaka 16 kuwa na akaunti.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: