Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Azinduka Kwenye Jeneza Muda Mchache Kabla ya Kuzikwa

Wafanyakazi katika hekalu la Kibudha nchini Thailand wamepatwa mshangao baada ya mwanamke aliyekuwa amepelekwa kwa ajili ya kuchomwa moto kama hatua ya mazishi kulingana na utamaduni wa nchi hiyo, kuanza kujitikisa na kukunja miguu akiwa ndani ya jeneza.

Tukio hilo ambalo limetokea Jumapili na kusambaa kwenye mitaandao ya kijamii jana Jumanne Novemba 25, 2025, tovuti ya AP imeeleza kuwa kaka yake ambaye hakupenda jina lake lijulikane, amesema dada yake huyo alikuwa anaugulia nyumbani kwa kulala kitandani kwa takribani miaka miwili kutokana na kuugua kwa muda mrefu, lakini alipokoma kupumua mwishoni mwa wiki iliyopita, familia walidhani kwamba alikuwa amefariki dunia.

Hivyo, walimpeleka hospitali iliyoko Bangkok, lakini maofisa wa hospitalini hapo walikataa kuwapokea kwa sababu hakuwa na cheti cha kifo.
Hivyo, amesema aliamua kumpeleka katika hekalu la Wat Rat Prakhong Tham pembezoni mwa jiji hilo, ambapo hutoa huduma ya uchomaji miili bila malipo.

“Ilikuwa wakati meneja wa hekalu alipokuwa akieleza jinsi ya kupata stakabadhi zinazohitajika ndipo tuliposikia sauti ya chini na tukaomba jeneza lifunguliwe,”amesema.

Bada ya kugundua alikuwa bado yupo hai, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 65 aliwahishwa hospitalini ambako ilibainika alikuwa na kiwango cha sukari mwilini, hali iliyosababisha udhaifu aliokuwa nao.

Vingozi wa hekalu hilo wameeleza kuwa watamgharamia mwanamke huyo fedha za matibabu ili kuendelea kurejea katika hali yake ya kawaida kiafya.

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: