Kamandi ya Kusini ya Jeshi la Marekani imesema imefanya mashambulizi dhidi ya boti tatu katika eneo la kimataifa la Bahari ya Pasifiki, ikidai zilikuwa zikisafirisha madawa ya kulevya.

Tukio hilo limesababisha vifo vya watu wanane, kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo iliyochapishwa kwenye mtandao wa X.
Chanzo; Dw