Rais Yoweri Museveni wa Uganda anayewania kuchaguliwa tena kuiongoza nchi hiyo katika uchaguzi wa Januari, 2026, hakujitokeza kushiriki mdahalo wa televisheni wa wagombea kiti cha urais uliofanyika usiku wa kuamkia leo.
Kwenye mdahalo huo wagombea watano kati ya wanane wanaoshiriki uchaguzi huo ndio walijitokeza ikiwemo mpinzani mkuu wa Rais Museveni, mwanamuziki aliyegeukia siasa, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine.
Kulingana na chama tawala cha NRM, Rais Museveni hakushiriki mdahalo huo kutokana na ratiba ngumu ya kampeni.
Chanzo; Dw