Washukiwa 32 wa Uhalifu wa Mtandaoni "Yahoo boys"
Wakamatwa Nchini Ghaba Kasoa–Tuba
Mamlaka ya Usalama wa Mtandao ya Ghana (CSA), kwa kushirikiana na vyombo vya usalama vya taifa, imewakamata washukiwa 32 wa uhalifu wa kimtandao, wanaojulikana kama “Yahoo boys”, katika oparesheni ya alfajiri eneo la Kasoa–Tuba.

Kwa mujibu wa taarifa ya CSA iliyotolewa Jumamosi, oparesheni hiyo ni sehemu ya juhudi za kudhibiti uhalifu wa mtandaoni nchini humo. Katika msako huo, maafisa wa usalama walikamata kompyuta mpakato 31 na simu za mkononi 15 zinazodaiwa kutumika katika shughuli za kihalifu.
Washukiwa wameshikiliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi, huku vifaa vilivyokamatwa vikifanyiwa uchunguzi wa kitaalamu wa kidijitali.
Chanzo; Cnn