Kitu cha ajabu kinachojulikana kama 3I/ATLAS, kinachothibitishwa na wanaastronomia kuwa ni kometi kutoka nje ya mfumo wetu wa jua, kinatarajiwa kupita karibu zaidi na Dunia tarehe 19 Desemba 2025, kikisafiri kwa kasi ya takriban maili 130,000 kwa saa.
Ingawa hakitaigonga Dunia, 3I/ATLAS kitapita umbali wa takriban maili milioni 170, jambo linalokifanya kuwa tukio adimu na la kihistoria katika sayansi ya anga.
Hiki ni kitu cha tatu tu cha aina yake kuwahi kugunduliwa kikitokea nje ya mfumo wa jua.

Wakati wanasayansi wengi wakisisitiza kuwa ni kometi ya kawaida, kauli ya mtaalamu mmoja wa Harvard imezua mjadala mkubwa, ikiongeza fumbo na msisimko kuhusu asili halisi ya mgeni huyu wa anga
Chanzo; Cnn