Serikali ya Afrika Kusini imetangaza rasmi janga la kitaifa kufuatia hali mbaya ya hewa katika baadhi ya maeneo ya nchi.
Mvua zimesababisha mafuriko makubwa yaliyoharibu nyumba na miundombinu na idadi ya vifo imeongezeka hadi kufikia watu 31, huku hali hiyo ikiendelea kuathiri maisha ya wananchi na kuharibu huduma muhimu.
Serikali ya nchi hiyo imesema hatua za dharura zinaendelea kuchukuliwa ili kusaidia waathirika wa janga hilo.
Chanzo; Dw