Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mwanajeshi Aliyepigwa Risasi Ikulu Afariki Dunia

Mmoja wa wanajeshi wawili wa ulinzi waliopigwa risasi katika Ikulu ya Marekani siku ya Jumatano amefariki dunia, Rais wa Marekani Donald Trump alisema.

Sarah Beckstrom, 20, alifariki dunia kutokana na majeraha, Rais Trump alisema Alhamisi jioni.

Mwanajeshi wa pili, Andrew Wolfe mwenye umri wa miaka 24, bado "anapigania maisha yake", Trump aliongeza.

Wote wawili walipigwa risasi kwa karibu katika Ikulu ya Marekani muda mfupi tu baada ya saa 14:00 za eneo (19:00 GMT) siku ya Jumatano.

Polisi wamemkamata mshukiwa mmoja kuhusiana na tukio hilo la ufyatuaji risasi, Rahmanullah Lakanwal, mwenye umri wa miaka 29 kutoka Afghanistan.

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: