Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

China Yazindua Ndege Yenye Huduma ya Upasuaji Angani

China yazindua hospitali yake ya kwanza inayoruka, ikileta huduma za matibabu za kisasa na upasuaji angani.

Ndege ya kwanza ya matibabu iliyotengenezwa nchini China, C909, sasa imeboreshwa kufanya upasuaji ndani ya ndege, ikiwemo upasuaji wa macho na masikio, pua, koo na sehemu ntingine za mwili.

Ndege hii ina chumba cha upasuaji kisafi cha Daraja la I na maeneo maalum yanayoweza kubadilishwa kwa ajili ya mashauriano, uchunguzi, mafunzo na upasuaji na Ikitengenezwa na Hospitali ya Macho na ENT ya Chuo Kikuu cha Fudan pamoja na COMAC,

Ndege hii ina uwezo wa uchunguzi wa mbali kwa teknolojia ya 5G, ikiruhusu wataalamu kuwahudumia wagonjwa moja kwa moja kwa wakati halisi.

Ikiwa imeundwa kwa ajili ya kupelekwa haraka, inalenga kupeleka huduma za afya za hali ya juu katika maeneo ya mbali ya China na kuchangia katika utoaji wa huduma za matibabu duniani kupitia anga.

 

Chanzo; Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: