Ndege zisizo na rubani za Ukraine zimeshambulia meli mbili za mafuta zinazojulikana kama 'shadow fleet' za Urusi zilipokuwa zikisafiri kupitia bahari nyeusi, maofisa wa Ukraine wamesema.
Picha zilizothibitishwa na BBC zinaonyesha ndege zisizo na rubani zikipita kwa kasi kwenye mawimbi hadi kwenye meli hizo, kabla ya kulipuka na kuwasha moto na kupelekea moshi mweusi kuonekana angani.
Meli za mafuta zilizolengwa zilitajwa na mamlaka ya Uturuki kama Kairos na Virat, zote zikiwa na alama ya Gambia. Zote mbili zilishambuliwa pwani ya Uturuki siku ya Ijumaa, na Virat iliripotiwa kushambuliwa tena siku ya Jumamosi. Hakuna majeruhi walioripotiwa.
Mashambulizi hayo yanaonekana kuzidishwa na Kyiv inapojaribu kuathiri mapato ya mafuta ya Urusi, ambayo ni muhimu kwa kufadhili vita vyake nchini Ukraine.
Chanzo; Nipashe