Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine amedai kwamba amekimbilia mafichoni baada ya kuvamiwa na wanajeshi nyumbani kwake.
Ameiambia DW kwamba wanajeshi waliagizwa na Mkuu wao Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa Rais Yoweri Museveni aliyepambana naye kwenye uchaguzi wa wiki iliyopita na ambaye anaamini alimshinda.
Wine amesema anahofia usalama wake huku akiishutumu familia ya rais kwa kuchukua hatua kinyume cha sheria, akiongeza kuwa wanafanya wanachokitaka na tayari amearifiwa kwamba wanataka kumdhuru.
Chanzo; Dw