Rais wa Marekani Donald Trump amefuta mwaliko wa Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney kujiunga na Bodi yake ya Amani.
Rais Trump ametangaza katika chapisho lake kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, bila ya kutoa sababu ya kuchukua hatua hiyo.
Awali Trump alilalama kwamba Carney ni mtu asiye na shukrani na kuongeza kuwa Canada ipo kwa sababu ya Marekani, huku akimuonya Carney kukumbuka hilo anapotoa matamshi yake.
Canada ni moja ya mataifa ambayo hayakuthibitisha kujiunga na Bodi hiyo iliyozinduliwa Alhamisi na Carney alisema kimsingi nchi yake inaweza kushiriki, lakini bado kuna masuala ambayo hayajakamilika
Trump alizindua rasmi bodi hiyo mpya jana katika Jukwaa la Uchumi Duniani huko Davos, Uswisi, ambayo wakosoaji wanaiona kama itakayokuwa mpinzani wa Umoja wa Mataifa.
Chanzo; Eatv