Rais wa Marekani Donald Trump anafikiria kupanua marufuku ya kusafiri kwenda Marekani kwa nchi 36 zaidi, nyingi zikiwa barani Afrika, kulingana na taarifa ya siri (cable) iliyonukuliwa na vyombo vya habari. Hatua hiyo inafufua sera tata ya marufuku ya safari iliyotekelezwa katika muhula wake wa kwanza, iliyozua upinzani mkubwa duniani.
Orodha ya nchi zinazoweza kuathirika ni pamoja na Tanzania, Uganda, Nigeria, Ghana, Ethiopia, DRC, Senegal, Zambia, Zimbabwe na nyingine nyingi. Endapo itatekelezwa, hatua hii inaweza kuathiri maelfu ya wasafiri, wanafunzi, wafanyabiashara na familia, huku ikizua mjadala mpya kuhusu uhamiaji, diplomasia na uhusiano wa Marekani na Afrika.
Chanzo; Cnn