Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Ujerumani Yaitaka Ubelgiji Kutumia Mali za Urusi

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema jana kuwa anaishinikiza serikali ya Ubelgiji kufikia makubaliano na Umoja wa Ulaya ya kutumia mali ya Urusi iliyofungiwa kuifadhili Ukraine.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Slovenia Robert Golob, Merz alisema lazima wafanye kila wawezalo ili kumaliza vita hivyo na kutumia mali ya Urusi ambayo kwa maoni yake ndio njia inayofaa.

Amesema anawasiliana na Waziri Mkuu wa Ubelgiji Bart De Wever kuhusu suala hilo.

Pia ameongeza kuwa anaelewa wasiwasi wa De Wever lakini pia wana hoja nzuri za kufikia malengo yao ya pamoja.

Wanachama wengi wa EU wataka mali ya Urusi itumike kufadhili Ukraine

Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya pamoja na wanachama wengi wa Umoja huo wanataka kutumia mali ya benki kuu ya Urusi isiyohamishika kuipa Ukraine mikopo, lakini Ubelgiji ambayo ni kituo kikuu cha kuhifadhia dhamana za Umoja wa Ulaya imesema inahofia kuwa hatua kama hiyo inaweza kusababisha visasi vya kisheria na kifedha kutoka Urusi.

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: