Ndege Ndogo ya Abiria imeliangukia gari dogo aina ya Toyota Camry baada ya kupata hitilafu ikiwa angani na kulazimika kutua kwa dharura barabarani huko Florida Marekani.
Imeelezwa kuwa Dereva wa gari hilo pamoja na Rubani na Abiria waliokuwepo kwenye Ndege hiyo wamenusurika kifo katika ajali hiyo na tayari Mamlaka ya Usafiri wa Anga Marekani (FAA) imeanza uchunguzi kubaini chanzo cha hitilafu iliyosababisha Ndege hiyo kutua kwa dharura.
Chanzo; Millard Ayo