Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Awauwa Wenzake na Kuwageuza Vipande vya Sabuni, Biskuti

Ule usemi wa rafiki yako ndiye adui yako unajidhihirisha kwa mwanamama kutokea nchini Italia aitwaye Leonarda Cianciulli ambaye aliwaua marafiki zake na kuwageuza vipande vya sabuni.

Akiwa na umri wa miaka 21 Leonarda aliolewa na mwanaume mlevi na asiye na kazi, kwa upande wake maisha yalikuwa magumu sana lakini kilichomvuruga Zaidi ni pale mtoto wake wa kiume Giuseppe kulazimishwa kujiunga na jeshi, ambapo mwanamke huyo aliingiwa na hofu kali akiamini kuna pepo wabaya wanataka kumdhuru mwanaye vitani.

Kufuatia na uteuzi huo Leonarda alichanganyikiwa ndipo akafanya uamuzi mgumu wa kutoa kafara za binadamu ili kumlinda mtoto wake ambaye alichaguliwa kwenda vitani, ambapo alianza kuwaalika marafiki zake nyumbani kupata mlo wa pamoja ili kutimiza adhma yake yake kafara.

Leonarda aliwaua marafiki zake wa karibu ambao ni Faustina Setti, Francesca Soavi na Virginia Cacioppo kwa nyakati tofauti inaelezwa kuwa alikuwa akiwaalika chakula cha jioni na wakati wa msosi alikuwa akiwachanganyia dawa za usingizi katika vinywaji vyao.

Pale mtu alipopatwa na usingizi alichukua shoka na kuanza kumgawanisha vipande kisha alimtumbukisa kwenye sufuria yenye kemikali na kumgeuzia kuwa sabuni lakini hakuishia hapo damu iliyobaki aliiacha ikauke kisha alichanganya na maziwa, sukari, ngano pamoja na mayai kisha kutengeneza biskuti ambazo alizigawa kwa majirani huku nyingine akiziuzwa dukani kwake.

Aidha ukatili huo haukudumu kwa muda mrefu kwani mmoja wa dada wa waathirika alimshutukia mwanamke huyo na kisha kuwaita polisi, na baada ya polisi kukagua nyuma walikuwa baadhi ya vitu vya waathirika hao.

Baada ya siri yake kufichuka, Leonarda alikamatwa na kufikishwa mahakamani mwaka 1946, ambapo alikiri makosa yake bila kusita. Mahakama ilimhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani pamoja na miaka mitatu katika hospitali ya magonjwa ya akili. Alifariki dunia mwaka 1970 akiwa chini ya uangalizi wa serikali.

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: