Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Fursa kwa Wanafunzi wa Kimataifa Wanaosomea Urusi Zajadiliwa Chuo Kikuu Cha RUDN

Moscow — Kuanzia Novemba 24 hadi 26, mji wa Moscow uliandaa Kongamano la kila mwaka la Mpango wa “Horizons of Opportunity,” lililowakutanisha wahitimu 150 bora kutoka maeneo mbalimbali ya Russia kujadili ushirikiano wa kimataifa na maendeleo ya taaluma.

Mojawapo ya matukio muhimu ilikuwa kikao cha pamoja kilichoitwa “Kufanya Kazi na Wahitimu wa Kimataifa: Kujenga Jamii Endelevu za Kitaaluma.” Kikao hiki kilijikita katika kuimarisha uhusiano wa muda mrefu na wahitimu wa kigeni wa vyuo vikuu vya Russia na kuunda njia madhubuti za kukuza taaluma zao ndani ya nchi.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Dmitry Ivanov, Mkurugenzi Mkuu wa World Youth Festival Directorate, alieleza juhudi zinazoendelea za kuwasapoti wahitimu wa kimataifa. Alisema kuwa idara yake inatilia mkazo kuendeleza mawasiliano thabiti na wahitimu na kupanua fursa za ushiriki wao.

Ivanov alisisitiza umuhimu wa programu za kielimu, akitaja kuwa Shule Nne za Majira ya Kiangazi ziliandaliwa mwaka 2025—zikilenga maafisa wa serikali na wabunge, wataalamu wa vyombo vya habari, wanamuziki na wabunifu, pamoja na walimu wa historia na lugha ya Kirusi kwa wageni.

Aligusia pia hatua mpya za kuunganisha jumuiya za kitaaluma, ikiwemo kuzinduliwa kwa International Content Center, kituo cha kudumu kwa ajili ya mafunzo, kubadilishana uzoefu na kuzalisha maudhui kwa pamoja na wanablogu vijana.

Katika mpango wa baadaye, Ivanov alitangaza kuwa kuanzia mwaka 2026 kutaanzishwa shindano la ruzuku kwa raia wa kigeni na mashirika ya kimataifa, hatua itakayowapa mfumo wa moja kwa moja wa kusaidia miradi yao.

Ameongeza kuwa miradi yote mikubwa tayari inazingatia mahitaji ya wanafunzi wa kimataifa, akiwaita “washirika muhimu” wanaoweza kuielezea Russia kwa dunia kwa njia ya ukweli, uwazi na ushahidi wa moja kwa moja.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Areg Aghasaryan, Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Vijana wa Kimataifa cha RUDN; Alexander Alimov, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kibinadamu wa Kimataifa na Mahusiano ya Kitamaduni katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia; Pavel Shevtsov, Naibu Mkuu wa Rossotrudnichestvo; na Konstantin Malyshev, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Vijana na Utalii katika Wizara ya Elimu na Sayansi ya Russia. Uwepo wao uliimarisha dhamira ya serikali kuendelea kushirikiana na mtandao wa wahitimu wa kimataifa.

Kuhusiana na mada hii: