Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Marufuku Mitandao kwa Watoto Chini Miaka 16 Yaanza Australia

Australia imeanza kutekeleza rasmi sheria inayopiga marufuku matumizi ya app 10 za mitandao ya kijamii kwa mtu yeyote aliye chini ya umri wa miaka 16 kuanzia Desemba 10.

Sheria hiyo, iliyopitishwa mwaka jana, imekuja kufuatia ongezeko la miito ya kuwepo kwa kanuni madhubuti kutokana na msururu wa matukio ya watoto kufanyiwa vitendo viovu na unyanyasaji wa kingono kupitia mitandao ya kijamii katika miaka ya karibuni nchini humo.

Marufuku hiyo inahusisha majukwaa kama Facebook, Instagram, Snapchat, Threads, TikTok, X, YouTube, Reddit, Kick na Twitch.

Kwa hatua hii, Australia imekuwa taifa la kwanza duniani kuweka marufuku ya kiwango hicho kwa watoto wa umri huo kutumia majukwaa ya mitandao ya kijamii.

Chini ya sheria mpya, waendeshaji wa majukwaa wana wajibu wa kuhakikisha hakuna mtoto chini ya miaka 16 anayeweza kutengeneza au kuendelea kutumia akaunti. Kampuni zitakazokaidi zitatozwa faini hadi dola milioni 49.5 za Australia, sawa na takribani dola milioni 32.8 za Marekani. Hakuna adhabu iliyowekwa kwa watoto wenyewe, wazazi au walezi.

Wakati baadhi ya wazazi wanaunga mkono hatua hiyo kama njia ya kuwalinda watoto dhidi ya maudhui hatarishi, tayari taarifa mtandaoni zimeanza kuonyesha njia zinazodaiwa kusaidia kukwepa marufuku hiyo.

Hata hivyo, mjadala umeibuka kuhusu kama inawezekana kuthibitisha kwa usahihi umri wa watumiaji kwenye mtandao. Kwa mujibu wa sheria mpya, jukumu hilo limewekwa kwa waendeshaji wa majukwaa, ambao sasa wanalazimika kuanzisha mifumo madhubuti ya uhakiki wa umri ili kutimiza matakwa ya sheria.

 

Chanzo; Wasafi

Kuhusiana na mada hii: