Rais wa Marekani Donald Trump ameibua mjadala mpana wa kimataifa baada ya kuweka hadharani ujumbe binafsi aliotumiwa na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, hatua iliyozua maswali kuhusu maadili ya diplomasia na faragha ya mawasiliano ya viongozi wa dunia.
Katika ujumbe huo, Rais Macron anaonekana kuzungumzia masuala nyeti ya kisiasa na kiusalama, akionyesha kuwa yeye na Trump walikuwa tayari wamefikia makubaliano kuhusu mzozo wa Syria na pia mipango ya ushirikiano wa pamoja kuhusu Iran. Hata hivyo, Macron alionyesha mshangao wake kuhusu msimamo wa Marekani juu ya Greenland, akisema hakuwa anaelewa kinachoendelea katika eneo hilo.
Chanzo; Global Publishers