Kenya imesema itatumia kiasi shilingi bilioni 15 hadi 20 sawa na dola milioni 155 za kimarekani kutoka kwenye kiwango ilichokusanya kupitia mauzo ya awali ya hisa za Kampuni ya Bomba la Mafuta ili kufanya upanuzi wa kiwanja chake cha ndege cha kimataifa kilichopo mjini Nairobi.
Hayo yameelezwa na Rais William Ruto wa nchi hiyo. Serikali ya Kenya ilitangaza wiki iliyopita kwamba imepata shilingi bilioni 106.3 kwa kuuza asilimia 65 ya hisa zake kwenye kampuni ya taifa ya Bomba la Mafuta na kwamba itatumia fedha hizo kufadhili miradi ya miundombinu ikiwemo barabara, reli na bandari.
Rais Ruto amesema upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta utakuwa mradi wa kwanza mkubwa utakaofadhiliwa chini ya mkakati huo mpya wa kutafuta fedha.
Chanzo; Dw