Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Trump Atia Saini Marufuku ya Kusafiri Nchi Zaidi ya Saba

Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumanne alipanua kwa kiasi kikubwa marufuku ya kusafiri kwa kuzuia watu kutoka nchi saba zaidi, ikiwemo Syria, pamoja na wamiliki wa pasipoti za Mamlaka ya Palestina, kuingia Marekani.


Hatua hii mpya inafanya idadi ya nchi zilizoathirika kufikia karibu 40, ambapo raia wake wanakabiliwa na vizuizi vya kuingia Marekani kwa sababu ya uraia wao pekee.


Nchi nyingine zilizoongezwa kwenye marufuku kamili ni Burkina Faso, Mali, Niger, Sierra Leone, Sudan Kusini na Laos. Vilevile, marufuku kwa sehemu yamewekwa kwa raia wa Nigeria, Ivory Coast, Senegal na mataifa mengine ya Afrika na Karibiani kama Angola, Benin, Gambia, Malawi, Mauritania, Tanzania, Zambia, Zimbabwe, pamoja na Tonga.

Nchi nyingine zilizoendelea kubaki kwenye marufuku ni Afghanistan, Chad, Kongo-Brazzaville, Eritrea, Haiti, Iran, Libya, Myanmar, Sudan na Yemen. Trump pia ameongeza masharti ya safari za kawaida kwa watu kutoka mataifa ya Magharibi.

 

 

Chanzo; Dw

Kuhusiana na mada hii: