Kabla ya kuingia Msikitini, Papa Leo alivua viatu na kuinama kidogo, kisha kutembezwa na Imamu wa Msikiti na Mufti wa Istanbul ndani ya msikiti huo unaowakusanya Waumini wapatao 10,000.
Hii ni ziara ya kwanza ya kigeni kwa Papa Leo tangu aingie madarakani ambapo pia anatazamiwa kuzuru Lebanon.
Papa huyo wa kwanza mwenye asili ya Marekani, anatarajiwa kuzungumza kwa mapana juu ya amani ya Mashariki ya Kati.
Chanzo; Dw