Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Trump Kuhamishia Ubabe Ufaransa Kisa Hormuz

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ataondoka madarakani hivi karibuni, kauli inayokuja wakati mvutano ukiongezeka kati ya Washington na washirika wake wa Ulaya.
Kauli hiyo ya Trump imetolewa jana Jumanne Machi 17, 2026 kufuatia uamuzi wa Ufaransa kukataa kushiriki katika juhudi za kijeshi zinazoongozwa na Marekani za kulinda mlango wa kimkakati wa mafuta wa Strait of Hormuz, katikati ya mzozo unaoendelea wa Iran.

Trump ametoa kauli hiyo akijibu msimamo wa Macron, ambaye amesisitiza kuwa Ufaransa si sehemu ya vita vinavyoendelea na haitashiriki operesheni za kijeshi, bali inaweza kuangalia uwezekano wa kushiriki katika juhudi za kurejesha utulivu baada ya vita.

Aidha, Trump amekuwa akizikosoa nchi kadhaa baada ya kukataa kuunga mkono operesheni za kijeshi kulinda mlango wa kimkakati wa mafuta wa Strait of Hormuz.

Kwa mujibu wa ratiba ya kisiasa ya Ufaransa, muhula wa sasa wa Macron unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, wakati nchi hiyo itakapofanya uchaguzi mkuu wa rais.

 

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: