Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema amechoshwa na mfululizo wa mikutano kuhusu namna ya kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine, na kwamba hadi sasa hakuna hatua madhubuti zinazopatikana.
Trump ametoa kauli hiyo wakati Ukraine ikilalamika kuwa Marekani bado inaishinikiza ikubali mpango unaojumuisha kuachia baadhi ya maeneo yake kwa Urusi kama masharti ya kufikia makubaliano ya amani.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Karoline Leavitt amesema Trump hataki kuendelea kusikia maneno matupu bila vitendo, akisisitiza kuwa anachotaka sasa ni kuona vita hivyo vinamalizika.
Chanzo; Itv