Utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump umeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC, kuachana na mipango yoyote ya kumchunguza na hata kumshtaki Rais Trump na maafisa wa utawala wake pale watakapomaliza muda wao mwaka 2029.
Utawala wa Trump umeitaka mahakama ya ICC kufanya marekebisho katika sheria yake ya msingi ili kuhakikisha haimchunguzi wala kumshtaki Rais huyo wa Marekani hapo baadaye.
Kulingana na afisa wa serikali ya Trump aliyezungumza kwa sharti la kutokutajwa jina, Utawala huo umeahidi vikwazo dhidi ya mahakama hiyo kama itashindwa pia kuachana na uchunguzi wa awali dhidi ya wanajeshi wa Marekani kutokana na vitendo vyao nchini Afghanistan na kesi dhidi ya viongozi wa Israel.
Chanzo; Dw