Baraza la Usalama la UN limeitaka Iran kusitisha mashambulizi dhidi ya nchi za Ghuba kupitia azimio lililopitishwa kwa kura 13, bila kulitaja jukumu la Marekani au Israel katika mgogoro huo.
Azimio hilo linashutumu pia vitisho vya Tehran dhidi ya safari za meli katika Mlango Bahari wa Hormuz.
Iran imelipinga vikali, ikisema hatua hiyo inatumika kuendeleza maslahi ya kisiasa ya Marekani na Israel.
Chanzo; Dw