Burundi imesema kwamba kusonga mbele kwa kundi la M23 chini ya wiki moja tangu kutiwa saini kwa makubaliano ya kusitisha vita nchini Kongo, ni "tusi kubwa" kwa Marekani na fedheha isiyo kipimo kwa Rais Donald Trump.
Hayo yamesema na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Burundi Edouard Bizimana aliyezungumza na Shirika la Habari la Ufaransa, AFP jana Jumatano.
Matamshi yake yanafuata uamuzi wa Burundi kuufunga mpaka wake na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo baada ya waasi wa M23 kusonga mbele na kuukamata mji wa kimkakati wa Uvira ulio karibu na mji wa kiuchumi wa Burundi, Bujumbura.
Bizimana ametoa mwito wa Rwanda kuwekewa vikwazo akiituhumu kutotaka amani kwa kuendelea kuliunga mkono kundi la M23 linalopigana vita na vikosi vya serikali ya Kongo.
Chanzo; Global Publishers