Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mapigano Makali Yaendelea Mashariki Mwa DRC

Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa huko Uvira mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wanakabiliana na jeshi la Kongo linaloungwa mkono na maelfu ya wanajeshi kutoka nchi jirani ya Burundi.

Shirika la Msalaba Mwekundu limesema kuwa raia wapatao 20 wakiwemo watoto wamejeruhiwa. Aidha, takriban wanajeshi 20 wa Burundi wameripotiwa kuuawa kwenye mapigano hayo tangu yalipozuka upya Jumatatu iliyopita. Hata hivyo, vyanzo kadhaa vya kijeshi vimeeleza kuwa kwa sasa wanajeshi wa Burundi wamewadhibiti waasi wa M23 na kuwasababishia pia hasara.

Pande zote mbili zinapigania udhibiti wa mji wa DRC wa Kamanyola ambao unapakana na mataifa ya Rwanda na Burundi na ambao kwa sasa unadhibitiwa na M23. Mapigano hayo yanaripotiwa ikiwa ni siku chache tu baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani kati ya rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi mjini Washington.

 

Chanzo; Dw

Kuhusiana na mada hii: