Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Tiktok Yasaini Ubia na Marekani Kukwepa Kufungiwa

TikTok, inayomilikiwa na kampuni ya China ya ByteDance, imetangaza kukamilisha makubaliano ya kuanzisha ubia mpya nchini Marekani unaomilikiwa kwa kiasi kikubwa na wawekezaji wa Kimarekani, hatua inayolenga kulinda data za watumiaji wa Marekani na kuepuka marufuku ya matumizi ya programu hiyo.

TikTok inatumiwa na zaidi ya Wamarekani milioni 200, na mpango huu unaweka msingi wa usalama wa data na mifumo ya kidijitali nchini humo.

Inaelezwa kuwa makubaliano hayo yanaashiria hatua muhimu baada ya miaka kadhaa ya mvutano wa kisiasa na kisheria ulioanza Agosti 2020, wakati Rais Donald Trump alipojaribu kuipiga marufuku TikTok kwa misingi ya usalama wa taifa hilo.

Kwa mujibu wa ByteDance, ubia huo mpya TikTok USDS Joint Venture LLC utahakikisha usalama wa data za watumiaji wa Marekani, programu na algoriti zake kupitia hatua madhubuti za faragha na usalama wa mtandao.

Chini ya mpango huo, wawekezaji wa Marekani na wa kimataifa watamiliki asilimia 80.1 ya ubia huo, huku ByteDance ikibaki na asilimia 19.9, wawekezaji wakuu watatu wanaosimamia ubia huo ni Oracle, Silver Lake na kampuni ya uwekezaji ya MGX ya Abu Dhabi, kila mmoja akimiliki asilimia 15.

 

 

Chanzo;Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: