Vijana kadhaa wa Kenya wamekamatwa wakiunga mkono maandamano yaliyopangwa kufanyika Disemba 09 nchini Tanzania. Wanasema walifika kwenye Ubalozi wa Tanzania mjini Nairobi kuonesha mshikamano na wenzao wa Tanzania. Maafisa nchini Tanzania waliyapiga marufuku maandamano ya umma na kwa jumla hapakuwa na watu waliojitokeza mitaani.
Chanzo; Dw