Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mkurugenzi wa FBI Atangaza Kujiuzulu

Dan Bongino ametangaza kuwa ataondoka katika wadhifa wake wa Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) mwezi Januari.

Katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa kijamii wa X, Bongino alimshukuru Rais Donald Trump, pamoja na Mkurugenzi wa FBI na Mwanasheria Mkuu wa Marekani, “kwa fursa ya kuhudumu kwa dhamira na uwajibikaji.”



Tangazo hilo linajiri baada ya Trump kusema mapema Jumatano kwamba aliyekuwa mtangazaji wa podikasti “alifanya kazi nzuri” akiwa ofisini, na kwamba “anataka kurejea kwenye kipindi chake.”

Bongino, aliyeteuliwa na Trump kushika wadhifa huo mwezi Februari, hapo awali alikuwa afisa wa polisi wa Jiji la New York na wakala wa huduma za ujasusi za Marekani, aliyekuwa na jukumu la kumlinda Rais wa zamani Barack Obama.

Katika miaka ya karibuni, alijipatia umaarufu mkubwa kupitia podikasti yake na kufanya mahojiano mbalimbali kwenye vyombo vya habari.

Akiwa mshirika wa karibu wa Trump, uteuzi wa Bongino ulionekana kuwashangaza wengi, kwani nafasi hiyo kwa kawaida hushikiliwa na maafisa wa taaluma ya muda mrefu wa FBI, ilhali yeye hakuwa na uzoefu wa awali ndani ya shirika hilo.

Chama cha Mawakala wa FBI, kinachowakilisha takribani mawakala 14,000 wa sasa na wa zamani, kilipinga uteuzi wake.

Akithibitisha uamuzi wake kupitia mitandao ya kijamii Jumatano, Bongino alisema:

“Nitaondoka katika wadhifa wangu wa FBI mwezi Januari. Nawashukuru Rais Trump, Mwanasheria Mkuu Pam Bondi, na Mkurugenzi Kash Patel kwa kunipa fursa ya kuhudumu kwa dhamira. Muhimu zaidi, nawashukuru ninyi, Wamarekani wenzangu, kwa heshima ya kuwatumikia. Mungu ibariki Marekani, na wote wanaoilinda.”

Kabla ya kujiunga na FBI, Bongino alikuwa ameunga mkpno taarifa potofu na nadharia za njama kuhusu madai ya uongo ya Trump kwamba alishinda uchaguzi wa mwaka 2020, pamoja na uchunguzi wa mabomu ya bomba uliotokea tarehe 6 Januari 2021.

Awali, Bongino aliwahi kudai kuwa kesi ya mabomu ya bomba ilikuwa “mpango wa ndani.”

 

 

Chanzo; Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: