Donald Trump pamoja na marais wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesaini Alhamisi mjini Washington makubaliano ya amani, huku mapigano makali yakiendelea kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23 huko jimboni Kivu Kusini, mashariki mwa Kongo.
Trump amesifu mkataba wa amani aloutaja kuwa "muujiza" baina ya marais Felix Tshisekedi wa Kongo na Paul Kagame wa Rwanda, uliotiwa saini leo Alhamisi jijini Washington. Mkataba huo unadhamiria kumaliza miongo mitatu ya machafuko mashariki mwa Kongo na katika kanda nzima ya Maziwa Makuu.
“Ni siku kuu kwa Afrika, siku kuu kwa dunia, leo tunafanikiwa pale ambapo wengi wameshindwa” - Trump
Chanzo; Tanzania Journal