Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mbunge Ajiuzulu Kisa Kutofautiana Mtazamo na Trump

Marjorie Taylor Greene ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya ubunge baada ya kutofautiana na kimtazamo na sera za mshirika wake wa karibu Rais wa Marekani Donald Trump.

Greene, amekuwa akitoa wito wa kutolewa kwa faili zinazohusiana na mnyanyasaji wa kingono marehemu Jeffrey Epstein na ukosoaji wa hivi karibuni wa baadhi ya sera za Trump ambazo anadai zimekuwa zikichochea hasira kali kwa umma.

Katika video ya dakika 10 iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii, Greene alisema alichochewa kujiuzulu kutokana na kutarajia kukubaliana na mpinzani wakati wa mchujo wa chama cha Republican anayeungwa mkono na Trump na uwezekano wa kiti cha Ubunge eneo hilo kunyakuliwa na Democrats katika uchaguzi wa katikati ya muhula wa mwaka ujao.

Pia alilalamika kwamba Bunge kwa kiasi kikubwa limetengwa tangu Trump arudi kwenye kiti cha urais mnamo Januari huku pia akilalamikia hali ya siasa za Marekani, akidai kuwa si Warepublican wala wabunge wa Democratic, hakuna mwenye nafasi ya kutatua matatizo ya taifa hilo, ikiwa ni pamoja na kupanda kwa gharama ya maisha.

Alisema katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, kwamba ataondoka kwenye Bunge la Marekani tarehe 5 Januari 2026.

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: