Waasi wa M23 wameanza kuondoka katika mji wa Uvira, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kufuatia agizo na shinikizo kutoka Marekani. Hatua hiyo inatazamwa kama dalili ya awali ya utekelezaji wa juhudi za kidiplomasia za kupunguza mvutano na kurejesha utulivu katika eneo hilo lililokumbwa na mapigano makali.
Chanzo; Cnn