Serikali ya Marekani, chini ya utawala wa Rais Trump, imetangaza rasmi kukamilisha mchakato wa kujiondoa katika Shirika la Afya Duniani (WHO) siku ya Alhamisi. Hatua hii inakuja ikiwa ni mwaka mmoja kamili tangu Rais Trump aliposaini amri ya mtendaji kuanza mchakato huo, ikiashiria mabadiliko makubwa katika uhusiano wa Kimataifa wa nchi hiyo kwenye sekta ya afya.
Afisa mwandamizi wa Idara ya Afya na Huduma za Binadamu (HHS) ameeleza kuwa uamuzi huo umetokana na madai kuwa WHO imepoteza mwelekeo wa dhamira yake ya msingi. Serikali imesisitiza kuwa katika matukio kadhaa, shirika hilo limekuwa likitenda kinyume na maslahi ya Marekani katika kulinda afya ya umma, jambo lililopelekea nchi hiyo kusitisha ushirikiano na ufadhili wake.
Chanzo; Itv