Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Israel Yadai Kumuua Waziri wa Ujasusi Iran

Mvutano wa kijeshi kati ya Israel na Iran umeingia hatua mpya kufuatia madai ya Israel kuwa imemuua Waziri wa Ujasusi wa Iran, Esmail Khatib, katika mashambulizi ya anga yaliyofanyika usiku wa kuamkia jana Jumanne.

Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, aliyesema operesheni hiyo pia ilimuua kiongozi wa juu wa usalama wa Iran, Ali Larijani.

Mamlaka za Iran zimethibitisha kifo cha Khatib na kueleza kuwa maziko yake yamefanyika leo.

Katz amesema mashambulizi hayo ni sehemu ya mkakati mpana wa kuwadhibiti viongozi wa vyombo vya usalama vya Iran, akisisitiza kuwa operesheni hiyo ilipangwa kwa umakini mkubwa.

Katika hatua hiyo, Israel pia imedai kumuua kamanda wa vikosi vya Basij, Gholamreza Soleimani, jambo linaloonesha ukubwa wa operesheni hiyo dhidi ya miundombinu ya kiusalama ya Iran.

 

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: