Afrika Kusini imethibitisha haitahudhuria Mkutano wa Kilele wa G20 wa mwaka 2026 Marekani baada ya maafisa wa Marekani kukataa kuipatia idhini rasmi (accreditation) hatua ambayo imezuia ushiriki wa ujumbe wa nchi hiyo.
Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini, Enoch Godongwana alisema nchi hiyo itasusia mikutano ya G20 wakati wa uenyekiti wa Marekani, lakini inapanga kurejea kushiriki mikutano ijayo itakayofanyika katika nchi nyingine.
Chanzo; Bongo 5