Zaidi ya wanafunzi 300 na waalimu 12 wametekwa nyara na watu waliojihami kwa silaha, katika shule ya Kikatoliki ya Mtakatifu Mary iliyopo kwenye jimbo la katikati mwa Nigeria la Niger. Kulingana na Chama cha Kikristo cha Nigeria, idadi hiyo imeongezeka kutoka 215 iliyotajwa Ijumaa baada ya uhakiki kufanyika.
Mamlaka zimesema vikosi maalumu vimeshaanza kufanya msako wa kuwaokoa wanafunzi hao. Tukio hilo ni la pili la aina hiyo ndani ya wiki moja baada ya wanafunzi wengine 25 kutekwa nyara katika jimbo la Kebbi. Serikali ya jimbo la Niger imetangaza kuzifunga shule nyingi wakati Rais Bola Tinubu amefuta shughuli zake za kimataifa ikiwemo ya kuhudhuria mkutano wa G20 nchini Afrika Kusini ili kulishughulikia suala hilo. Hadi sasa hakuna kundi lolote la wanamgambo lililotangaza kuhusika na utekaji huo
Chanzo; Dw