Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló, amekamatwa na watu wenye silaha leo, siku 3 baada ya uchaguzi ambao mgombea mkuu wa upinzani aliondolewa.
Embaló na mpinzani wake, Fernando Dias, wote wametangaza kushinda, huku Dias akipinga matokeo hayo. Tume ya uchaguzi imesema matokeo ya mwisho yatatangazwa kufikia Alhamisi.
Lakini wanajeshi wa Guinea-Bisau tayari wametangaza mapinduzi
Guinea-Bissau, ambako wananchi zaidi ya asilimia 65 walijitokeza kupiga kura, ina historia ndefu ya mapinduzi na misukosuko ya kisiasa.
Chanzo; Bbc