Vyanzo kadhaa nchini Marekani vimesema Rais Donald Trump alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais Nicolas Maduro wa Venezuela na kumtaka kiongozi kusalimu amri kwa kuondoka madarakani.
Kwenye mazungumzo hayo ya Novemba 21 yaliyodumu chini ya dakika 15, Trump alimwambia Maduro kwamba ana "wiki moja pekee ya kuondoka Venezuela akiwa pamoja na familia yake na kwenda kwenye nchi atakayochagua."
Inaarifiwa pia Trump alikataa sehemu kubwa ya mapendekezo ya Maduro ikiwemo kuondolewa kwa vikwazo vyote vya Marekani vinavyomkabili yeye na maafisa wengine wa serikali. Marekani imekuwa ikiongeza shinikizo kwa kiongozi huyo inayemtuhumu kuhusika na ufadhili wa biashara haramu ya dawa za kulevya, madai ambayo Maduro ameyapinga mara zote.
Mwenyewe amesema Marekani inatumbia mabavu kumng´oa madarakani ili ipate nafasi isiyo na upinzani ya kuvuna rasilimali za Venezuela hasa hazina kubwa ya mafuta iliyo nayo.
Chanzo; Dw