Mgombea urais wa Uganda Bobi Wine ameiambia CNN kuwa uchaguzi ujao si wa kidemokrasia bali ni vita binafsi dhidi yake, akidai vyombo vya usalama vimeachiliwa kumshambulia yeye na wafuasi wake. Waandishi wa CNN walirushiwa mabomu ya machozi walipokuwa wakiripoti moja ya mikutano yake ya kampeni.
Bobi Wine alimshutumu Rais Yoweri Museveni, akisema: “Museveni anaiona Uganda kama mali yake binafsi na sisi kama watumwa wake.” Kauli hiyo nzito inaongeza joto la kisiasa huku taifa likielekea kwenye uchaguzi wenye mvutano mkubwa.
Chanzo; Cnn