Polisi nchini Uganda imesema imemkamata mbunge na afisa mwandamizi wa chama kikuu cha upinzani, National Unity Platform (NUP), kwa tuhuma za kuhusika katika vurugu za uchaguzi ambazo zilisababisha vifo vya takriban watu saba.
Mbunge huyo, Muwanga Kivumbi, ambaye pia ni makamu wa rais wa NUP, anadaiwa kuhusika na machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi.
Polisi imethibitisha kukamatwa kwa Kivumbi kupitia chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa X, na kusema kuwa mbunge huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.
Chama hicho kinaongozwa na mwanamuziki maarufu aliyeingia kwenye siasa, Bobi Wine, ambaye amekuwa mafichoni tangu wiki iliyopita kutokana na kile anachodai kuwa ni vitisho na ukandamizaji kutoka kwa vyombo vya usalama.
Chanzo; Dw