Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Aliyemuua Waziri Mkuu Atupwa Jela Maisha

Kijana aliyemuua aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe kwa kutumia bunduki ya kutengenezwa nyumbani, amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani, kwa mujibu wa taarifa ya shirika la utangazaji la umma la Japan, NHK, iliyotolewa leo Jumatano Januari 21, 2026.

Hukumu hiyo inahitimisha kesi iliyodumu kwa miaka kadhaa kuhusu mauaji yaliyolishtua taifa la Japan; nchi inayojulikana kwa viwango vya chini vya uhalifu wa kutumia silaha za moto na pia kuyaelekeza macho ya umma kwenye dhehebu la kidini lenye ushawishi mkubwa.

Mshitakiwa, Tetsuya Yamagami, alimfyatulia risasi Shinzo Abe mchana kweupe mwaka 2022, wakati kiongozi huyo wa zamani alipokuwa akitoa hotuba ya kampeni barabarani katika mji wa Nara, magharibi mwa Japan.

Bunduki iliyotumika iliripotiwa kutengenezwa na Yamagami mwenyewe nyumbani.

Shinzo Abe alikuwa amejiuzulu wadhifa wa uwaziri mkuu mwaka 2020 kutokana na sababu za kiafya, lakini aliendelea kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Japan.

Anatajwa kama waziri mkuu aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Japan, na mchango wake uliendelea kuonekana hata baada ya kuondoka madarakani.

Mamia ya watu walijipanga nje ya mahakama mjini Nara wakisubiri nafasi ya kushuhudia kesi hiyo, huku maafisa wakilazimika kutumia mfumo wa bahati nasibu kugawa viti vichache vilivyokuwepo ndani ya ukumbi wa mahakama.

Uongozi wa Abe unaonekana na wengi kama kipindi cha mwisho cha uthabiti wa kisiasa nchini Japan.

Alihudumu kama waziri mkuu kuanzia mwaka 2006 hadi 2007, na tena kuanzia 2012 hadi 2020.

Katika mihula yake miwili, Abe alibadilisha kwa kiasi kikubwa sera za usalama za Japan, hatua iliyozua mjadala kuhusu msimamo wa nchi hiyo kama taifa lisilotumia nguvu za kijeshi.

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: