Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Netanyahu Aomba Msamaha kwa Rais wa Israel

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amewasilisha ombi la kusamehewa kwa Rais wa nchi hiyo Isaac Herzog.

Ofisi ya rais ilisema Herzog atapokea maoni kutoka kwa maafisa wa haki kabla ya kulizingatia "ombi hilo lisilo la kawaida ambalo lina athari kubwa".

Netanyahu amekuwa akikabiliwa na kesi kwa miaka mitano iliyopita kwa tuhuma za hongo, ulaghai na uvunjaji wa uaminifu kuhusiana na kesi tatu tofauti. Hata hivyo, anakanusha kutenda kosa lolote.

Alisema katika ujumbe wa video kwamba angependelea kuona mchakato huo hadi mwisho, lakini masilahi ya kitaifa "yalidai vinginevyo".

Mapema mwezi huu, Rais wa Marekani Donald Trump alimtaka Herzog "kumsamehe kabisa" waziri mkuu.

 

Chanzo; Bbc

Kuhusiana na mada hii: