Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mkuu wa Nato, Urusi Inaweza Kutushambulia

Urusi inaweza kushambulia nchi iliyo katika jumuiya ya Nato ndani ya miaka mitano ijayo, mkuu wa muungano huo wa kijeshi wa Magharibi amesema katika onyo jipya kabisa.

"Urusi tayari inaimarisha kampeni yake ya siri dhidi ya jamii zetu," Mark Rutte alisema katika hotuba yake nchini Ujerumani.

"Lazima tuwe tayari kwa kiwango cha vita ambacho babu na bibi zetu walistahimili"

Alirejelea kauli kama hizo kuhusu nia ya Urusi iliyotolewa na mashirika ya kijasusi ya Magharibi, ambazo Moscow imezipuuzilia mbali ikidai ni hofu zao tu.

Onyo la Rutte linakuja wakati Rais wa Marekani Donald Trump akijaribu kukomesha uvamizi kamili wa Urusi dhidi ya Ukraine, uliozinduliwa Februari 2022.

Mapema mwezi huu, Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema nchi yake haikupanga kuingia vitani na Ulaya, lakini ilikuwa tayari ikiwa Ulaya inataka au kuanzisha vita.

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: